Fukwe Zanzibar zatengewa Sh661 milioni

Fukwe Zanzibar zatengewa Sh661 milioni

Dodoma. Katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imetenga Sh661 milioni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya ujenzi wa fukwe zilizoathirika na mabadiliko ya tabianchi upande wa Zanzibar.

 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis amesema hayo leo Jumanne  Mei 14, 2024 alipojibu swali la mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Suleiman Haroub Suleiman.

Mbunge huyo alihoji Serikali ina mpango gani wa kutengeneza fukwe za bahari zilizoathirika upande wa Zanzibar.

Naibu Waziri Khamis amesema kwa mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imepanga kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya ujenzi wa fukwe zilizoathirika kwa upande wa Zanzibar.

Amesema Sh661 milioni zimetengwa kwa ajili ya miradi hiyo na kuwa kati ya fedha hizo, Sh300 milioni zitatumika kukamilisha ujenzi wa matuta ya kuzuia maji ya bahari kuingia sehemu ya mashamba ya mpunga katika Shehia ya Kwa mgogo, Kusini Pemba katika ufukwe wa Sipwese.

“Sh361 milioni ni kwa ajili ya kufanya tathmini katika eneo la Nungwi ili kusanifu namna bora ya kudhibiti uharibifu unaoendelea,” amesema.

Katika swali la nyongeza, Suleiman amehoji Serikali ina mpango gani wa kwenda kurekebisha fukwe zilizoathirika na mabadiliko ya tabianchi.

Pia, amesema kuna fukwe zina takataka nyingi, akihoji Serikali ina mpango gani wa kuzidhibiti.

Naibu Waziri, Khamis amesema zipo hatua kadhaa ambazo zimechukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema hatua hizo ni kuanzisha miradi inayoenda kutatua changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, kutoa elimu na kuchukua hatua kuona namna wanavyoweza kushurutisha wananchi kuepukana na mambo yanayoweza kusababisha athari.

Amesema tayari hatua kadhaa ikiwamo ya kufanya usafi katika maeneo ya mji wa Zanzibar ili kuondoa takataka, zimechukuliwa.

Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima amesema kwa sababu ya mvua kubwa zilizonyesha baadhi ya mito imepanuka kufikia mita 300.

Kutokana na hilo, amehoji licha ya kutolewa fedha, waziri ana mpango gani wa kuongozana naye kwenda kuangalia athari za mito hiyo?

Khamis amesema yuko tayari kuambatana na mbunge huyo kwenda kuangalia athari na kuwasaidia wananchi.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Popular
Swahili News Editor

MGAO WA MAJI WAWATESA WAZANZIBARI

Wananchi wengi hasa katika maeneo ya Mjini Unguja, wanalalamikia ukosefu wa maji safi na salama huku Mamlaka ya Maji Zanzibar ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ujuzi na wataalam katika masuala ya uandisi wa Maji na fani nyengine.Continue Reading