Dk Biteko: Rais Samia kawapaisha wanawake sekta ya madini

Dk Biteko: Rais Samia kawapaisha wanawake sekta ya madini

Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kufungua fursa za kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutilia mkazo ushirikishaji wa wanawake katika uchimbaji wa madini wenye tija.

Dk Biteko amesema  hayo jijini Dar es Salaam juzi aliposhiriki kongamano maalumu kuelekea maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa  Machi 8, 2025.

Amesema kwa sasa kuna ongezeko kubwa la wanawake wanaoshiriki kwenye sekta ya madini ambayo kwa muda mrefu imeendelea kutawaliwa na wanaume.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, watu 6,030,575 wanajihusisha na shughuli mbalimbali za mnyororo wa thamani katika sekta ya madini na kati yao, wanawake ni 3,094,647 sawa na asilimia 51.3 ya watu wote wanaojihusisha na uchimbaji mdogo wa madini hususan katika sekta ndogo ya uziduaji.

Aidha, kati ya wachimbaji wadogo milioni 1.5, asilimia 27 kati yao wachimbaji hao ni wanawake.

“Katika kukuza ushiriki wa wanawake katika sekta hiyo, Rais Samia anasisitiza kutoa kipaumbele kwa wanawake kushiriki shughuli zote za kiuchumi kwa kuwapatia  fursa za elimu na kumiliki rasilimali zilizopo kama kupata elimu, mikopo yenye masharti nafuu na kupata vifaa na vitendea kazi na kushiriki katika vikao mbalimbali vya maamuzi,” amesema Dk Biteko.

Amesema ushiriki wa wanawake katika sekta ya madini, ni msingi muhimu wa kukuza mnyororo wa thamani ndani ya jamii.

 “Kutambua na kuthamini mchango wao, kunachangia maendeleo endelevu katika sekta hiyo,”amesema Dk Biteko.

Pia, amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake kushiriki kikamilifu kupitia utekelezaji wa sera, sheria na taratibu mbalimbali.

Kupitia Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake (2023) na Sheria ya Madini (2017), pamoja na kanuni za ‘Local Content,’ Serikali inahakikisha wanawake wanapata fursa na rasilimali zinazowawezesha kushiriki kikamilifu sekta ya madini.

 Amesema hatua za uwezeshaji wa kifedha na kitaaluma zinaendelea kutekelezwa kupitia taasisi za Serikali na wadau ikiwamo Kamisheni ya Madini Tanzania na Umoja wa Wachimba Madini Wanawake Tanzania (Tawoma).

Katika hafla hiyo, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amewapongeza waandaaji wa mkutano huo kwa juhudi zao za kuendeleza ushiriki wa wanawake katika sekta ya uziduaji.

“Nimshukuru Rais Samia kwa juhudi zake za ushawishi wa kutaka mabadiliko ya Sheria ya Madini (2017), ambayo imeongeza ushiriki wa wanawake katika sekta ya madini,” amesema Mavunde.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaidi Ali Khamis amesema maono ya Rais Samia ya kuunda taasisi inayoshughulikia masuala ya wanawake moja kwa moja ni hatua muhimu katika kuwawezesha wanawake, hasa  wanaofanya kazi katika sekta ya madini.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Popular
Swahili News Editor

MGAO WA MAJI WAWATESA WAZANZIBARI

Wananchi wengi hasa katika maeneo ya Mjini Unguja, wanalalamikia ukosefu wa maji safi na salama huku Mamlaka ya Maji Zanzibar ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ujuzi na wataalam katika masuala ya uandisi wa Maji na fani nyengine.Continue Reading

Africa: Rwanda Gets a Grip Of Marburg, But Mpox ‘Not Yet Under Control’
Top News
Chief Editor

Africa: Rwanda Gets a Grip Of Marburg, But Mpox ‘Not Yet Under Control’

Africa: Rwanda Gets a Grip Of Marburg, But Mpox ‘Not Yet Under Control’

Monrovia — The Rwanda Minister of State responsible for Health, Dr. Yvan Butera, cautioned that while the country is beginning to see positive signals in its fight against the Marburg virus, the outbreak is “not yet over”. He, however, expressed hope that  “we are headed in that direction”. The minister said the epidemiology trend, since the disease was first discovered in the country more than a month ago, is moving towards fewer cases.

Dr. Butera, who was giving updates during an online briefing yesterday, said in the past two weeks, only two deaths were recorded while 14 people recovered from the disease. He said Rwanda was expanding its testing capacity with 16,000 people already inoculated against the disease.

The priority right now, Butera said, is “rapid testing and detection”.

Marburg is a highly virulent disease transmitted through human-to-human contact or contact with an infected animal. The fatality rate of cases, which has varied over the period, is more than 50%, according to the World Health Organization.  WHO said the highest number of new confirmed cases in Rwanda were reported in the first two weeks of the outbreak. There’s been a “sharp decline” in the last few weeks, with the country now tackling over 60 cases.

At Thursday’s briefing, a senior official of the Africa Centers for Disease Control, Dr. Ngashi Ngongo, said mpox – the other infectious disease outbreak that countries in the region are fighting – was been reported in 19 countries, with Mauritius being the latest country to confirm a case. He said although no new cases have been recorded in recent weeks in several countries where outbreaks occurred previously –  including Cameroon, South Africa, Guinea, and Gabon – Uganda confirmed its first Mpox death. This, he said, is one of two fatalities reported outside Central Africa.

Dr. Ngashi revealed that there was an increase in cases in Liberia and Uganda. He said mpox cases were still on an upward trend.

“The situation is not yet under control.”

Source: allafrica.com

Continue Reading