Bajeti 2025/26 Zanzibar yapaa
Makadirio hayo ni ongezeko la Sh1.621 trilioni sawa na asilimia 31 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2024/2025 ya Sh5.182 trilioni.Continue Reading
Hii ni tovuti ya idhaa ya Kiswahili inayokuletea habari na makala kutoka Zanzibar, Tanzania, Afrika na duniani kote kwa lugha ya Kiswahili.
Makadirio hayo ni ongezeko la Sh1.621 trilioni sawa na asilimia 31 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2024/2025 ya Sh5.182 trilioni.Continue Reading
Dira ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni kuhakikisha inatengeneza mifumo ya kuvutia zaidi ya wanasoka wa kike milioni moja kucheza katika ligi za ngazi mbalimbali hapa nchini.Continue Reading
Tanzania imekuwa ni miongoni mwa nchi ambazo bado zinakabiliwa na changamoto ya udumavu wa kimo na akili kwa watoto.Continue Reading
Dar es Salaam. Uuzaji wa Malighafi ya kahawa kumeifanya Afrika kuendelea kutumia fedha nyingi katika kuingiza kahawa iliyosindikwa huku ikinufaika kiduchu na mauzo ya nje.
Imeelezwa kuwa Nchi za Afrika kwa pamoja hupata wastani wa dola bilioni 2.5 (Sh6.4 trilioni) kwa mwaka kutokana na mauzo ya kahawa nje ya bara, kati ya Dola za Marekani bilioni 500 zinazopatikana kwenye soko la dunia kwa mwaka.
Haya yamesemwa leo Februari 21, 2025 na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akifungua mkutano wa tatu wa nchi 25 wazalishaji wa kahawa katika Bara la Afrika.
Katika mkutano huu zinajadiliwa fursa zilizopo na namna ambayo vijana wanaweza kujumuishwa katika sekta ya kahawa.
Bashe amesema fedha hizo kiduchu zinatokana na asilimia 90 ya kahawa ya Afrika kusafirishwa kama malighafi, huku thamani yake ikiongezwa nje ya bara la Afrika.
“Hili linamaanisha kuwa Afrika inanufaika kwa sehemu ndogo sana ya mnyororo wa thamani ya kahawa. Sehemu yenye faida kubwa zaidi ya mnyororo huu ni usindikaji na ongezeko la thamani ambalo kwa kiasi kikubwa hufanywa katika nchi zinazoagiza kahawa. Hii inapunguza mapato yetu na nafasi za ajira kwa watu wetu,” amesema Bashe.
Amesema jambo hilo linaathiri hata wauzaji wadogo kwani wanauza kilo 1 ya kahawa kwa wastani wa Dola za Marekani 4 hadi 7 (Sh10,317 hadi Sh18,054) na kisha kuinunua kwa wastani wa Dola za Marekani 15 hadi 20 (Sh38,680 hadi Sh51,000) kwa kilo moja baada ya kusindikwa.
“Hili ni kosa kubwa kwa bara letu. Afrika ndicho chimbuko la kahawa. Huu ni urithi wetu ambao tunapaswa kuulinda na kuhakikisha unastawi,” amesema Bashe.
Amesema Afrika inachangia asilimia 11 tu ya uzalishaji wa kahawa duniani, ambayo ni nusu ya kiwango tulichokuwa tukizalisha miaka ya 1960 wakati ambao uzalishaji wa kahawa duniani unazidi kuongezeka kila mwaka Afrika inashuhudia kupungua kwa uzalishaji.
Jambo hilo linahitaji uwekezaji wa haraka kutoka sekta ya umma na binafsi ili kurejesha sehemu ya soko lililopotea.
“Ni lazima sasa tuache kulalamika na kuwategemea wafadhili kukuza sekta yetu ya kahawa na kilimo kwa ujumla. Ni jambo lisiloeleweka kuwa tunasafirisha kahawa yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3 (Sh7.75 trilioni) na kuagiza kahawa iliyosindikwa yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 50 (Sh130 trilioni).
“Tunahitaji kuweka malengo ya kuongeza uzalishaji wetu kufikia angalau asilimia 20 ya uzalishaji wa kahawa duniani ifikapo 2030,” amesema Bashe.
Amesema kwa sasa, Afrika inaagiza nusu milioni ya tani za kahawa kwa matumizi ya ndani kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 6 (Sh15.6 trilioni) kila mwaka.
Amesema ili kuhakikisha wakulima wa ndani wananufaika zaidi ni vyema kuwekeza katika viwanda vya usindikaji vya kiwango kidogo na kikubwa katika nchi zote zinazozalisha na kutumia kahawa Afrika.
Bashe amesema ni wakati sasa kwa nchi hizi kushikamana na kuacha kutegemea misaada na kudai haki katika biashara ya kimataifa na badala yake kuungana kama bara na kujadiliana kwa pamoja badala ya kufanya kazi kwa kutengana.
Kwa nini vijana hawalimi kahawa
Katika hili Bashe amesema changamoto ya Kupanda na kushuka kwa bei ya kahawa duniani kumeifanya sekta hiyo kukosa mvuto kwa vijana hivyo ili kushughulikia hilo uwekezaji unapaswa kufanyika hasa katika uongezaji wa thamani ndani ya nchi, kuongeza biashara ya kahawa na uwekezaji katika usindikaji.
“Afrika ina soko kubwa la watumiaji lenye watu bilioni 1.5 lakini sehemu kubwa ya kahawa inayotumiwa barani huagizwa kutoka nje baada ya kusindikwa nje ya bara letu. Hili linapaswa kubadilika kwa kuhamasisha usindikaji wa ndani na kuifanya kahawa kuwa sehemu ya utamaduni wetu,” amesema Bashe.
Amesema vijana wanapaswa kuwa kiini cha sekta ya kahawa kwa kuwawekea mbinu rafiki za kilimo na kuweka kipaumbele katika ustawi wa wakulima.
“Kwa kufanya hivi tunaweza kuhakikisha kuwa sekta ya kahawa Afrika inastawi kwa vizazi vijavyo. Mafanikio haya hayawezi kupatikana bila ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, na vyama vya kahawa,” amesema Bashe.
Amesema hilo linawezekana kwa sababu Afrika ina ardhi yenye rutuba, rasilimali za maji na nguvu kazi ya vijana na hakuna sababu ya Afrika kushindwa kuongeza uzalishaji wake wa kahawa na kufaidi kikamilifu thamani ya zao hilo.
“Ni wakati wa kubadili mwelekeo kutoka kuwa wasafirishaji wa malighafi kwenda kwenye kuongeza thamani na kutengeneza bidhaa zilizokamilika. Ni lazima tuongeze biashara kati yetu wenyewe kutoka asilimia 15 hadi asilimia 50 jambo ambalo haliepukiki, na hii inapaswa kuwa moja ya maazimio hapa Dar es Salaam,” amesema Bashe.
Amesema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuweka malengo kwamba ifikapo mwaka 2030 nchi zote zinazotumia kahawa Afrika zinunue kahawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wa Kiafrika.
Amesema jambo hilo linawezekana na litafungua fursa nyingi za ajira kwa vijana na uwekezaji katika uchumi wa mzunguko.
Tanzania inavyovutia vijana
Akizungumzia kinachofanyika Tanzania, Waziri Bashe amesema katika kuvutia vijana katiki kilimo cha kahawa tayari imeanzisha mradi wa kuuza kahawa mitaani kupitia migahawa inayotembea.
Mradi huu unatekelezwa chini ya programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT) ambapo vijana wanapatiwa vibanda vya kahawa vilivyo na vifaa vyote na mtaji wa kuanzia ili wawe wauzaji wa kahawa katika miji yetu.
“Pia Tanzania imejizatiti kuleta mageuzi katika sekta ya kahawa kupitia hatua kama vile kuimarisha taasisi za utafiti wa kahawa, kutoa ruzuku za pembejeo kwa wakulima, na kukuza ushiriki wa vijana kupitia programu ya BBT,” amesema Bashe.
Mkurugenzi bodi ya kahawa
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Primus Kimaryo amesema sekta hii ina uwezo mkubwa wa kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi, kukuza ubunifu na kuinua nafasi ya Afrika katika soko la kahawa la kimataifa.
Hata hivyo, licha kuwa ni kitovu cha masoko ya kahawa ya Arabica na Robusta, Bara la Afrika halijaweza kutumia kikamilifu uwezo wa kahawa yake.
“ Wito wangu kwa serikali za Afrika ni kuwekeza katika ongezeko la thamani, kuimarisha biashara ya kahawa kati ya nchi za Afrika,”
“Kuwawezesha wajasiriamali vijana na kuwaleta vijana katika mustakabali kwa kuwawezesha na kuwapa stadi, fedha na fursa za kubadili sekta ya kahawa kuwa injini inayoleta ajira na ukuaji wa kiuchumi,” amesema Kimaryo.Continue Reading
Uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) uliotoa agizo kwa Tanzania kufuta adhabu ya kifo iliyotolewa kwa Ladislaus Chalula na kumwondoa katika orodha ya wanaosubiri kunyongwa, umechochea upya mjadala kuhusu mustakabali wa adhabu ya kifo nchini.Continue Reading
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeonya uwepo wa hali mbaya ya hewa kwa siku tano katika mikoa mitano nchini pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.Continue Reading
Katika juhudi za kubadilisha taswira ya utalii wa Tanzania, Kampuni ya Maendeleo Hospitality Ventures (MHV) inayosimamiwa na kundi la wawekezaji kutoka Marekani, imetangaza mpango wa kujenga hoteli ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano katika Kijiji cha Robanda, karibu na Lango la Fort Ikoma, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.Continue Reading
Dar es Salaam. Wakala ya Barabara Tanzania (Tanroads) umepokea tuzo ya kimataifa kutokana na mchango wake wa kuboresha usalama wa barabara (safer road).
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega na Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mohamed Besta kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana Februari 17, 2025 wamepokea tuzo ya heshima katika mashindano ya kimataifa ya usalama wa barabara.
Tuzo hiyo iitwayo iRAP Gary Liddle Memorial Trophy, ilitolewa kutokana na mchango wa Tanroads, katika kuboresha usalama wa barabara ili kupunguza hatari za ajali na kuhakikisha usalama wa watumiaji wote wa barabara, kupitia mpango wa Ten Step Plan Tanzania.
Hafla ya kutolewa kwa tuzo hiyo ilifanyika jana Jumatatu Februari 17, 2025, katika mkutano wa Ten Steps to 2030 for Safer Road Infrastructure Side Event uliofanyika katika Palais des Congres, Marrakech nchini Morocco, ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 4 wa mawaziri kutoka mataifa mbalimbali duniani kuhusu usalama barabarani.
Tanroads ilikuwa ni miongoni mwa washindani watano walioteuliwa kutoka nchi 11, baada ya kushindanishwa na taasisi nyingine 12 duniani. Mbali na Tanroads, taasisi nyingine zilizofikia hatua ya mwisho katika tuzo hii ni kutoka nchi za India, Australia, Peru, na Saudi Arabia.
iRAP Gary Liddle Memorial Trophy hutolewa kwa mamlaka na wakala za barabara duniani zinazofanya juhudi kubwa za kuondoa barabara zenye hatari kwa watumiaji wake.
Tuzo hii ni ya kudumu, ikiwa ni heshima kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya iRAP, Gary Liddle AO, aliyefariki mwaka 2023.Continue Reading
Wakati Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ikisema vipindi vya ongezeko la joto vinatarajiwa kuendelea kujitokeza Februari mwaka huu, wataalamu wa afya wameshauri mambo ya kuzingatia katika unywaji, uvaaji, mtindo wa maisha, na ulaji, wakisisitiza kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta.Continue Reading
Jumuiya ya Ulaya (EU) imetoa ufadhili wa zaidi ya Sh17. 8 bilioni kwa asasi za kiraia 11 nchini Tanzania, kwa lengo la kukuza demokrasia kwa kujenga jamii yenye uwazi, haki, na ujumuishi zaidi, kwa kuimarisha sauti za wananchi na taasisi.Continue Reading
Zanzibar Investment News Tanzania Investors Ltd © 2025