Tanzania inauza asilimia tano tu ya asali yake nje ya nchi
Sababu zinazokwamisha ni pamoja na kutokidhi viwango vinavyoweza kuifanya ikidhi kuuzwa katika soko la kimataifa.Continue Reading
Hii ni tovuti ya idhaa ya Kiswahili inayokuletea habari na makala kutoka Zanzibar, Tanzania, Afrika na duniani kote kwa lugha ya Kiswahili.
Sababu zinazokwamisha ni pamoja na kutokidhi viwango vinavyoweza kuifanya ikidhi kuuzwa katika soko la kimataifa.Continue Reading
Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kukamilika kwa jengo la abiria uwanja wa ndege wa Arusha kutapunguza msongamano na kuongeza utulivu wa abiria.
Makonda amesema hayo baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ukarabati wa jengo la abiria katika uwanja huo ambalo ameagiza likamilike haraka na lianze kutumika Septemba mosi.
Akizungumza baada ya kukagua jengo hilo, Makonda amesema kukamilika mapema kwa jengo hilo kutawezesha abiria kuwa na mahali pazuri pa kusubiri usafiri na kupunguza msongamano uliopo sasa.
Amesema shauku ni uwanja huo kukamilisha maboresho ikiwemo uwekaji wa taa za kuongozea ndege ambayo yatauwezesha kutumika kwa saa 24, tofauti na inavyotumika sasa saa 12 pekee kutokana na kutokuwepo kwa taa.
“Tumetembelea hapa kuona kazi inayoendelea na ni shauku yetu uwanja utumike kwa saa 24,na kupitia Sh7 bilioni zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kuweka taa za kuongozea ndege, tunaamini mradi huo utasaidia uwanja utumike kwa saa 24,” amesema
“Kuhusu kuweka taa tumepata taarifa mkandarasi ameshapatikana na mkataba umesainiwa wa miezi 12 ila tumezungumza na mkurugenzi jana, walau miradi ukamilike ndani ya miezi minane,” aliongeza Makonda
Meneja wa uwanja huo, Godfrey Kaaya, amesema mradi wa jengo la abiria na miundombinu yake utagharimu Sh8 bilioni na umefikia asilimia 90.
Amesema jengo la abiria linalotumika kwa sasa lina uwezo wa kuhudumia abiria 150 wakati lile linalokamilishwa likitarajiwa kubeba abiria 1,000 kwa wakati mmoja.
“Tumejipanga kuhakikisha Septemba lianze kutumika kwani limeshafikia asilimia zaidi ya 90,” amesema.
Kuhusu mradi wa taa za kuongozea ndege, Godfrey amesema mkandarasi ameshapatikana na ameshaanza kazi za awali za usanifu na kuwa watasimamia mradi huo utekelezeke chini ya miezi 12, ili kiwanja hicho kiweze kutumika kwa saa 24.
“Kwa sasa kiwanja hiki kinatumika kwa saa 12 tu, ila ni kiwanja cha ndege cha pili kwa miruko mingi ya ndege Tanzania bara baada ya Julius Nyerere,” amesema
“Tuna miruko karibu 150 kwa siku. Kwa mfano kipindi hiki cha msimu wa utalii, zinakuja ndege 75 na zinaondoka ndege 75 na ndege zote ni ndani ya saa 12, tofauti na viwanja vingine ambavyo vinahudumia ndege kubwa,” ameongeza
Kuhusu ongezeko la abiria, meneja huyo amesema kwa kipindi cha mwaka 2019 kabla ya Uviko -19, kulikuwa na watalii wengi akitolea mfano Julai mwaka huo, walivyopokea abiria zaidi ya 38,000 akilinganisha na Julai 2024 walivyohudumia abiria zaidi ya 45,000.
“Hao abiria zaidi ya 45,000 asilimia zaidi ya 90 ni watalii, hivyo ni kiwanja muhimu hasa katika biashara ya utalii,” amesema.
Maboresho ya uwanja huo wa ndege ni muhimu kwani asilimia kubwa ya watalii hupita Kaskazini huku Arusha ikitumika kama lango kuu, hivyo kukamilika kwa miradi hiyo kutachochea kasi ya maendeleo kwa kiwango kikubwa.
Kwa sasa mwonekano wa kuingia katika uwanja huo umeanza kubadilika kufuatia maboresho yaliyofanywa, likiwemo eneo la maegesho ya magari ambalo limekamilika na linatumika.
Barabara ya kuingia katika uwanja huo imeboreshwa tofauti na ilivyokuwa awali, likiwa limebaki jengo la abiria linalokamilishwa na uwekaji wa taa.
Kama una maoni kuhusu habari hii, tuandikie ujumbe kupitia WhatsApp: 0765864917.Continue Reading
Unyeti wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania na rundo la wajibu unaotegemea utashi wa wizara nyingine, ndiyo sababu iliyotajwa na wadau kuifanya wizara hiyo iwe mapito ya muda mfupi kwa kila anayeteuliwa.Continue Reading
Kigwangalla, ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha wabunge wanaopiga vita usugu wa dawa Tanzania, amesema kuna haja ya kuwashirikisha wadau ili kuhakikisha sera na mipango ya Serikali inatekelezwa.Continue Reading
Dar es Salaam. Tumbaku ikishika nafasi ya pili katika mauzo ya bidhaa za asili nje ya nchi mwaka 2023, wadau wanashauri itafutwe njia mbadala ya kukausha zao hilo hasa kwa wakulima wadogo ili kuepusha ukataji miti unaoweza kuligharimu Taifa.
Hata hivyo, Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) katika mazungumzo na Mwananchi imesema tayari kuna aina mbili za mbegu zinazotumia hewa na jua kukauka zimeanza kutumiwa na wakulima katika baadhi ya mikoa.
Ripoti ya Takwimu za Msingi Tanzania 2023 inaeleza kuongezeka uzalishaji wa tumbaku nchini ni moja ya sababu ya mauzo ya nje ya nchi kukua zaidi ya mara mbili, kati ya mwaka 2021 hadi 2023.
Inaelezwa katika ripoti hiyo kuwa, kukua kwa mauzo kutoka Sh291.4 bilioni mwaka 2021 hadi Sh824.9 bilioni mwaka 2023 kunaifanya tumbaku kushika nafasi ya pili katika mauzo ya bidhaa za asili nje ya nchi na kuleta mapato mengi nchini, ikiipiku korosho ambayo mwaka 2023 ilishika nafasi hiyo.
Ripoti hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inafafanua kuwa siyo mauzo tu ya zao hilo yaliyoongezeka, bali hata bidhaa zinazotokana na tumbaku nazo uzalishaji wake umeongezeka.
Uchambuzi unaonyesha uzalishaji sigara uliongezeka kutoka sigara bilioni 7.02 mwaka 2021 hadi bilioni 11.86 mwaka 2023.
Ongezeko la uzalishaji sigara unaifanya kuwa bidhaa ya pili miongoni mwa baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa viwandani zilizoainishwa na ripoti upande wa Tanzania Bara kati ya mwaka 2019 hadi 2023 ikitanguliwa na bidhaa za rangi.
Agosti 8, 2024 Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alimweleza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa, kama si mvua za El-Nino, Tanzania ingekuwa mzalishaji mkubwa wa tumbaku duniani kwa kuwa hivi sasa inashika nafasi ya pili ikitanguliwa na Zimbabwe.
“…Umechukua uongozi wa nchi yetu uzalishaji wa tumbaku ukiwa ni tani elfu 65 na malengo yetu kwa sasa ilikuwa ni kuzalisha tani 170,000 hadi tani 200,000 lakini tumefikisha tani 122,000,” alisema Bashe.
Mtaalamu wa Uchumi na Biashara kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Aurelia Kamuzora amesema Taifa linapaswa kuangalia namna linavyoweza kutumia zaidi fursa ya uzalishaji na uuzaji tumbaku nje ya nchi ili kujiingizia fedha za kigeni.
Amesema fursa hiyo inaweza kutumika zaidi hasa katika kipindi hiki ambacho baadhi ya nchi duniani zinapunguza uzalishaji kutokana na kampeni zinazofanywa kupiga marufuku matumizi ya sigara katika maeneo yao.
“Sisi tunaweza kuimarisha uzalishaji kwa kufanya utafiti kuangalia sehemu ambazo watu wanaweza kulima zaidi tumbaku na kufanya uzalishaji ili kutumia fursa iliyopo,” amesema.
Kuhusu uzalishaji wa sigara kuongezeka, Profesa Kamuzora amesema athari zake kwa watumiaji ni bayana na huainishwa hata kwenye pakiti, akisema kisanyansi kitu chochote kinapotumiwa kupita kiwango kinaweza kumuathiri mtu.
“Kama mtu unakunywa supu ya nyama yenye mafuta mengi kila siku utaishia kupata tatizo, kila kitu unapotumia kwa wingi kina madhara,” amesema Profesa Kamuzora.
Hata hivyo amesema ni vyema kuangalia kama nikotini inaweza kuwaathiri hadi wakulima, kwa kufanya tafiti katika moja ya mkoa unaozalisha kwa wingi tumbaku na kulinganisha na ule ambao hauzalishi.
Amesema moja ya kitu kinachoweza kuangaliwa ni umri wa mtu kuishi.
Ukataji miti
Ukataji miti kwa ajili ya kupata kuni za kukaushia tumbaku ni suala linalojadiliwa hapa na pale, kwamba kadri uzalishaji unavyoongezeka ndivyo nchi inakuwa kwenye hatari ya kuwa jangwa.
Profesa Kamuzora amependekeza kuwapo mipango ya njia zinazoweza kutumika kukausha zao hilo bila kutumia kuni zinazosababisha ukataji miti.
“Kuna baadhi ya kampuni niliona zinaotesha miti kwa ajili ya kufidia uharibifu nafikiri tunahitaji kujipanga zaidi kwa kuangalia wapi tunaweza kurekebisha, ikiwemo kupanda miti kwa wingi,” amesema.
Akizungumza na Mwananchi, Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB), Stanley Mnosya amesema njia pekee ya kuzuia ulimaji tumbaku kuathiri mazingira ni kuangalia namna ya kudhibiti ukataji miti.
Amesema kwa sasa wamebadili majiko ya kukaushia tumbaku kwa kuondoa yenye uwezo wa kuingiza magogo na kuweka yanayotumia matawi matawi ya miti pekee.
Amesema wameingia mkataba wa miaka mitatu na moja ya kampuni itakayokuwa ikiwajengea wakulima majiko.
“Lakini ukiacha hili, tuna mbegu mpya aina mbili za tumbaku ambazo zitakuwa hazihitaji moto kukaushia, badala yake zitatumia hewa na mwanga wa jua,” amesema Mnosya.
Amesema mbegu inayokaushwa kwa kutumia hewa huhitaji kivuli, hivyo mkulima atafunika na nyavu na kuacha sehemu ya kupitisha hewa.
Pia kama mtu ana miti ya kivuli ana uwezo wa kuweka tumbaku chini yake na ikakauka vizuri.
“Mbegu hizi tayari zimeanza kutumika katika maeneo ya Iringa, Singida na baadhi ya sehemu ya Tabora, lengo letu ni kuona mwaka huu asilimia 30 ya tumbaku yote itokane na mbegu hizi na tutakuwa tukiongeza kidogokidogo hadi zao hili nchi nzima litakapokuwa linatokana na mbegu hizi,” amesema.
Kutokana na baadhi ya tumbaku kuendelea kukaushwa kwa moto amesema kupitia Mfumo wa Usimamizi wa Misitu unaotegemea Jamii (CBFM) wanalinda watu kutoingia kiholela kukata misitu, bali kwa kufuata utaratibu ambao unaenda sambamba na watu kufundishwa namna ya kuvuna misitu.
Amesema kuna kampeni maalumu inayowataka wakulima kupanda miti 500 anapolima hekta moja, huku vikundi vya kinamama na vijana vimeundwa kusimamia na kutunza miti inayopandwa.
Mikakati mingine
Wakati hayo yakifanyika, bajeti ya Wizara ya Kilimo ya mwaka 2024/2025 inataja mkakati katika zao hilo ni kuratibu upatikanaji wa tani 127,316 za mbolea na kusambaza kwa wakulima kwa mpango wa ruzuku.
Hilo litaenda sambamba na usambazaji wa viuatilifu lita 236,329 na pakiti 1,664,286, vifungashio belo 11,709 na nyuzi 166,429 kwa ajili ya kuimarisha uzalishaji wa tumbaku.
Mbolea ya NPK (10:18:24) itaagizwa na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na kusambazwa kwa wakulima wa tumbaku.
“Bodi ya Tumbaku Tanzania itajenga mabani ya kisasa 2,353 katika mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita, Kigoma, Ruvuma, Katavi, Mbeya, Songwe, Iringa, Morogoro na Mara. Mabani hayo yatasaidia kupunguza upotevu wa majani, kuongeza ubora wa tumbaku na kutunza mazingira,” imeeleza wizara katika bajeti hiyo.Continue Reading
Dar es Salaam. Sakata la kuzuiwa mikutano ya hadhara na ile ya ndani ya vyama vya siasa limechukua sura mpya, baada ya Jeshi la Polisi Tanzania kukanusha zuio la Polisi Wilaya ya Mbagala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Kanusho hilo la Polisi Makao Makuu linatokana na taarifa ya Polisi Mbagala kwenda kwa chama cha ACT-Wazalendo kuzuia kufanyika kwa mkutano wa hadhara waliopanga kufanyika leo Jumatatu, Agosti 12, 2024 katika Kata ya Charambe, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.
Barua ya Polisi Wilaya ya Mbagala kwenda kwa ACT-Wazalendo ya leo Jumatatu, pamoja na mambo mengine imesema: “…napenda kukujulisha kuwa mikutano yote ya hadhara na ya ndani imezuiliwa hadi hapo yatakapotolewa maelekezo mengine.”
Baada ya barua hiyo mijadala imeshika kasi mitandaoni, huku wadau wa kisiasa wakikumbusha kile kilichotokea mwaka 2016 kwa mikutano ya hadhara kupigwa marufuku na kuruhusiwa ile ya ndani.
Zuio hilo la mikutano liliwekwa wakati wa utawala wa awamu ya tano, baada ya utawala wa awamu ya sita kuingia madarakani ukiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan uliliondoa na mikutano kurejea.
Mwananchi lilizungumza na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kutaka kujua undani wa zuio hilo la Polisi Mbagala ambapo amesema kinachojitokeza ni hali ya jeshi hilo kujichanganya, hakuna tamko rasmi lilotolewa la kufuta mikutano ya hadhara na ile ya ndani.
“Kilichotokea naona kama Polisi wamejichanganya, hakuna tamko rasmi lilotolewa la kuzuia mikutano ya hadhara na ya ndani kwa kuwa Jeshi la Polisi lina ngazi aulizwe msemaji wake anaweza kuwa na majibu sahihi,” amesema Jaji Mutungi.
Katikati ya mijadala hiyo, saa 8:20 mchana, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, David Misime akatoa taarifa kwa umma akisema: “Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa halijapiga marufuku kufanyika mikutano ya nje ya hadhara na ile ya ndani, ili mradi inafuata matakwa ya sheria za nchi.”
“Kilichopigwa marufuku ni mkusanyiko uliokuwa umeitishwa na viongozi wa Chadema huko jijini Mbeya, kwa kivuli cha kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani,”ilieleza taarifa hiyo.Continue Reading
Serikali ya Tanzania ipo kwenye mazungumzo na kampuni hiyo, ikiwa na muda wa miezi sita kutafuta suluhu kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.Continue Reading
Hilo limesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, baada ya kutembelea na kukagua bidhaa za kilimo na ufugaji leo Agosti 9, 2024 katika maonyesho ya wakulima Nanenane katika viwanja vya Dole Kizimbani, Unguja.Continue Reading
Mchora katuni maarufu na mtangazaji wa Clouds Media Group nchini Tanzania, Ally Masoud maarufu Masoud Kipanya, amemfungulia kesi Mtangazaji wa Crown Media Ltd, Burton Mwemba Mwijaku, akidai fidia ya Sh5.5 bilioni kwa kumkashifu na kumshushia hadhi na heshima yake kupitia maandishi aliyochapisha kwenye mitandao ya kijamii.Continue Reading
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kuzitangaza kimataifa bandari nyingine zilizopo maeneo tofauti na ile ya Dar es Salaam ili ziweze kuhudumia nchi mbalimbali zinazopitisha mizigo yake Tanzania.Continue Reading
Zanzibar Investment News Tanzania Investors Ltd © 2025