Tanzania yaendeleza mikakati kufikia usawa wa kijinsia
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UN Women, Dk Mitra Sadananda amesema ahadi ya Tanzania ya kuendeleza usawa wa kijinsia imewezesha wanawake kiuchumiContinue Reading
Hii ni tovuti ya idhaa ya Kiswahili inayokuletea habari na makala kutoka Zanzibar, Tanzania, Afrika na duniani kote kwa lugha ya Kiswahili.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa UN Women, Dk Mitra Sadananda amesema ahadi ya Tanzania ya kuendeleza usawa wa kijinsia imewezesha wanawake kiuchumiContinue Reading
Kundi la watu wenye ulemavu kutoka vyama vya United Democtratic Party (UDP), Democratic Party (DP), Tanzania Labor (TLP) na Union for Multiparty Democracy (UMD) limeonyesha kuridhishwa na miundombinu rafiki ya huduma za afya inayotolewa nchiniContinue Reading
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Baraka Leonard kuwa Katibu wa Bunge, kuchukua nafasi ya Nenelwa Mwihabi, aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.Continue Reading
Zaidi ya watoto 400 wenye umri wa kati ya miaka saba na 17 kutoka mikoa ya Kigoma, Mwanza, Dar es Salaam na Unguja walishiriki katika mikutano hiyo.Continue Reading
Walimu wa shule za awali, msingi na sekondari nchini Tanzania watapata mafunzo maalumu kuhusu utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika masomo yao ya darasani. Hii ni sehemu ya maboresho ya mitaala ya mwaka 2023 yenye lengo la kuingiza masuala haya kwenye mitalaa ya shule.Continue Reading
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema ni kiu yake kuona taasisi za Serikali zinakuwa mfano wa kulipa kodi vyema mbele ya walipakodi wengine.Continue Reading
Dodoma. Walimu wanne na mfanyabiashara mmoja wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwatapeli wananchi kwa kuwadanganya kuwekeza katika sarafu za kimtandao (cryptocurrency), kisha kutoweka na fedha walizowekeza.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, ametoa taarifa leo Septemba 11, akieleza kuwa watuhumiwa walikamatwa Septemba 7, 2024, katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza kufuatia malalamiko ya wananchi waliodhulumiwa.
Ingawa Misime hakuwataja walimu hao wala shule wanazotoka, amefafanua kuwa watuhumiwa wamehusishwa na ulaghai kwa kufungua mifumo ya kampuni bandia ili kuvutia uwekezaji wa wananchi.
Majina ya baadhi ya kampuni hizo ni MEME BANK, DIGITAL WEALTH INTERNATIONAL, OCTOQUANT AI TRADING, NPAMA FUND, MINDFUL TRADE, na CELESTRIAL TG CRYPTOCURRENCY.
Misime amesema kuwa matapeli hao huanzisha kampuni hizo na kuwapa wawekezaji wa awali fedha kidogo kama faida ili kuvutia wengine wawekeze zaidi.
Hata hivyo, baada ya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha, kampuni hizo hufungwa na matapeli hao kutoweka mtandaoni, na kuwafanya wawekezaji kushindwa kuwasiliana nao.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuepuka kujiingiza kwenye udanganyifu huu, kwani teknolojia ya uwekezaji wa sarafu za kimtandao bado haijaidhinishwa rasmi nchini.
Wananchi wanashauriwa kutoa taarifa wanapoona ulaghai wowote unaohusisha uwekezaji mtandaoni au biashara za aina hiyo, ili kuepusha kupoteza fedha zao.
Misime amesisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha uhalali wa makampuni au watu wanaohamasisha biashara za mtandaoni kabla ya kujiingiza, kwani wengi wamejikuta wakiibiwa fedha kutokana na kuingia kwenye matapeli wa mtandaoni.Continue Reading
Wiki ya mafunzo ya amali, inayofanyika Chuo cha Amali Mwanakwerekwe, Unguja, ina lengo la kuwajengea wanafunzi mwamko wa kuchagua fursa za ujuzi. Maonyesho haya yameanza Septemba 9 na yataendelea hadi Septemba 15, 2024.Continue Reading
Ujenzi wa vituo vya umahiri nchini Tanzania vinatajwa kuleta mapinduzi katika utoaji wa elimu na kuzalisha wataalamu wa kutosha katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), usafirishaji, utengenezaji wa bidhaa za ngozi pamoja na nishati jadidifu.Continue Reading
Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) inakusudia kuanza kuwasajili wakulima wote wa kahawa nchini ili kukidhi matakwa ya sheria mpya ya soko la Jumuiya ya Ulaya (EU).Continue Reading
Zanzibar Investment News Tanzania Investors Ltd © 2025