Upatikanaji maji Mwanza bado changamoto
Takwimu za Sensa ya Majengo ya Mwaka 2022 zinaonyesha asilimia 24.9 ya majengo milioni 13.9 (13,907,951) ya Tanzania Bara yana huduma ya maji, huku hali ikiwa tofauti kwa majengo milioni 10.Continue Reading
Hii ni tovuti ya idhaa ya Kiswahili inayokuletea habari na makala kutoka Zanzibar, Tanzania, Afrika na duniani kote kwa lugha ya Kiswahili.
Takwimu za Sensa ya Majengo ya Mwaka 2022 zinaonyesha asilimia 24.9 ya majengo milioni 13.9 (13,907,951) ya Tanzania Bara yana huduma ya maji, huku hali ikiwa tofauti kwa majengo milioni 10.Continue Reading
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Mugisha Nkoronko ametaja vipaumbele atakavyoanza navyo katika uongozi wake wa miaka miwili.Continue Reading
Dar es Salaam. Jamii imeaswa kutofungama na makundi ya watu yenye lengo la kubomoa umoja uliojengeka baina yao kwa kusambaza taarifa zisizo sahihi na kuibua chuki na taharuki.
Wito huo umetolewa leo Septemba 28, 2024 jijini Dar es Salaam na Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu katika siku ya pili ya mkutano wa 53 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania.
Zungu amesema kila mtu katika jamii anapaswa kujiona ana wajibu wa kulinda amani na kuisaidia Serikali katika kuhakikisha wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa amani wanachukuliwa hatua za kisheria.
Ametoa wito kwa viongozi wa dini kuiombea nchi na kuendelea kuhubiri masuala ya amani na upendo kwa waumini.
Vilevile ameipongeza jumuiya hiyo kwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya athari ya kuchanganya masuala ya dini na siasa.
“Kuchanganywa kwa masuala ya dini na siasa kunaweza kuleta mkanganyiko na kuzalisha mianya ya ama wanasiasa kuitumia dini vibaya au watu wa dini kutumia siasa vibaya kwa ajili ya masilahi yao binafsi,” amesema.
Katika mkutano huo, Zungu pia amezungumzia mmomonyoko wa maadili hasa kwa vijana, akitaja utandawazi na matumizi yasiyo sahihi ya mitandao kama baadhi ya visababishi.
Amesema ili kuondokana na changamoto hiyo ni muhimu wazazi kuhakikisha wanahimiza na kusimamia watoto kupata elimu ya darasani pamoja na ya dini.
Vilevile amewataka viongozi wa dini kuhakikisha jamii inapata mafunzo sahihi ya dini ili kuwajenga kuwa na hofu ya Mungu.
“Elimu sahihi ya kimaadili mnayowapa watoto wenu ndiyo inayojenga jamii imara yenye kujenga waumini wenye maadili. Mtu hawezi kuwa mpenzi wa Mungu kisha akaacha kufanya wema kwa viumbe wengine hasa wanadamu,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Elimu Msingi, Abdi Maulid amesema mtoto akipata elimu ya darasani na ya dini itasaidia kuzalisha wanataaluma katika fani mbalimbali wenye maadili.
Amir wa jumuiya hiyo, Khawaja Ahmad amesema madhehebu hayo yamekuwa yakifanya mkutano kila mwaka kwa lengo la kuwakutanisha waumini na kuwakumbusha wajibu wao kama binadamu hapa duniani ikiwemo kumcha Mungu.
Amesema mkutano huu unalenga kuongeza hofu ya Mwenyezi Mungu, kuhimiza kuepukana na maovu, kuchochea moyo wa huruma na upendo na kuwakumbusha waumini kuendeleza tamaduni ya kuisaidia jamii katika nyanja mbalimbali, ikiwemo utoaji wa huduma za afya, elimu na misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji bila ya kujali itakadi ya imani zao.
“Vilevile kuwaelimisha na kuwahimiza vijana kuwa na mienendo bora ya kimaisha na kuwa raia wawajibikaji kwa nchi yao, na kuwa viongozi waadilifu katika jamii kwa mustakabali wa jamii na Taifa bora,” amesema.Continue Reading
Kwa kipindi cha miaka minne, Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) imesajili meli za nje 800 na za ndani 40, hivyo kukusanya Sh10.167 bilioni.Continue Reading
Aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa, ameieleza Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, jinsi alivyoshiriki mchakato wa kutoa eneo kwa ajili ya kupewa aliyekuwa Askofu wa kwanza wa dayosisi hiyo na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, hayati John Sepeku.Continue Reading
Wakati Zanzibar ikitimiza miaka 60 ya elimu bila malipo leo Jumatatu, Septemba 23, 2024, wanazuoni na wanataaluma wametoa mapendekezo namna elimu hiyo inavyotakiwa kuboreshwa, ili kuendana na mahitaji ya sasa ya kidunia.Continue Reading
Wadau wa mazingira nchini Tanzania wameishauri Serikali, kuanzisha wakala utakaowezesha wakazi wa vijijini kupata nishati safi ya kupikia kwa gharama ya chini kama ilivyo kwa umeme.Continue Reading
Wakati Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (Zipa) ikisajili miradi mipya ya uwekezaji 353 yenye thamani ya Dola za 5.5 bilioni za Marekani (Sh14.99 trilioni), uwepo wa amani na kuimarika kwa miundombinu ya kiuchumi na huduma za kijamii vinatajwa kuvutia mitaji mikubwa ya uwekezaji kutoka nje.Continue Reading
Tanzania ina wabunifu karibu 200 na wenye kampuni za kiteknolojia wako 33 zinazosaidiwa na Serikali.Continue Reading
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuhakikisha Mkoa wa Kigoma unaunganishwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwisho mwa mwaka 2024.Continue Reading
Zanzibar Investment News Tanzania Investors Ltd © 2025