Balozi wa Marekani Tanzania alivyozindua kampeni dhidi ya Ukimwi

Balozi wa Marekani Tanzania alivyozindua kampeni dhidi ya Ukimwi

Dar es Salaam. Ili kudhibiti kuenea kwa Ukimwi Tanzania, wadau wa maendeleo  na ustawi wa jamii, wamezindua kampeni ya kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia jitihada za Serikali katika kupambana na ugonjwa huo.

Hatua hiyo inakuja wakati Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi (THIS) ya mwaka 2022/2023, unaonyesha Tanzania ina watu milioni 1.5 wanaoishi na VVU, maambukizi mapya ya mwaka yamepungua kwa asilimia 16.7 kutoka 72,000 kwa mwaka 2016/17 hadi 60,000  2022/23), huku maambukizi yakiongezeka maradufu miongoni mwa wasichana wenye umri wa miaka 15-24.

Hivyo wadau hao wanakusanya fedha kupitia kampeni ya Kilimanjaro Challenge ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Tume yaTaifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids)  ili kuhamasisha juhudi za kupambana na ugonjwa huo.

Katika kutekeleza hilo, kampeni ya GGM Kili Challenge 2024 ambayo inahusisha kupanda na kuzunguka Mlima Kilimanjaro kila mwaka fedha hizo zitakusanywa, huku lengo ni kupata kiasi cha Dola milioni 1 (zaidi ya Sh 2.6 bilioni).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle amesema ahadi za michango zinatarajiwa kukamilishwa katikati  ya Julai 2024.

“Kama wengi wenu mnavyofahamu, Mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Ukimwi, unaojulikana kama Pepfar, umekuwa nguzo katika mapambano ya kimataifa dhidi ya Ukimwi kwa zaidi ya miaka 20, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003,” amesema.

Amesema Pepfar imewekeza nchini, ikiunga mkono miradi mbalimbali ya kudhibiti janga hili huku ikiwa imepiga hatua, ambapo zaidi ya watu milioni 1.5 wanapata matibabu ya kuokoa maisha kupitia msaada.

Aidha, wamepunguza kwa kiasi kikubwa vifo vinavyohusiana na Ukimwi na idadi ya maambukizi mapya.

“Hata hivyo, sasa tupo katika hatua ambapo uendelevu ni muhimu kwa sababu Pepfar haikuwahi kuwa suluhisho la kudumu; ilibuniwa kukidhi hitaji la dharura,  Tanzania imepiga hatua kubwa katika kudhibiti janga la Ukimwi, viwango vya maambukizi mapya vimepungua kwa kiasi kikubwa, pamoja na vifo vinavyohusiana na Ukimwi,” amesema.

Aidha Balozi Battle amezisifu GGML na TACAIDS kwa kushirikiana kwenye kampeni kama hiyo inayosaidia Serikali kupambana na kuenea kwa Ukimwi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Duan Archery amesema michango inathamani na itasaidia kufikia lengo la ‘kufikia sifuri’, ambalo ni kutokuwepo kwa maambukizi mapya, kutokuwepo kwa ubaguzi, na kutokuwepo kwa vifo vinavyohusiana na Ukimwi.

Pia,Makamu wa rais wa AngloGold Ashanti wa Masuala ya Uendelevu na Mambo ya Ubia (Afrika), Simon Shayo amesema vikundi mbalimbali vimefaidika na kampeni hiyo, ikiwa ni pamoja na watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Moyo wa Huruma, ambacho pia kinawatunza watoto wengine walio katika mazingira magumu.

“Kundi la kwanza la watoto waliokulia katika kituo hicho sasa wanasoma vyuoni, wakiwemo wawili wanaosoma digrii za udaktari,” amebainisha Shayo.

Hata hivyo, akizungumza katika hafla hiyo, Jumanne Isango akimwakilisha Dk Jerome Kamwela, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, amesema  fedha zote zitakazokusanywa zinagawanywa kwa mashirika yanayohusiana na Ukimwi akisema vita inahitaji msaada  zaidi wa ndani, hasa wakati michango ya kigeni inapopungua.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

ZAA to audit ground handlers
Popular
Investment News Editor

Zanzibar Airport Authority to audit ground handlers

Unguja. The Zanzibar Airports Authority (ZAA) is set to conduct an audit on ground handling companies that currently operate at the Abeid Amani Karume Airport with effect from Monday. The week-long audit is set to include Transworld, ZAT and the newcomer Dnata Zanzibar who were licensed in June plus exclusive rights to manage Terminal 3 building by ZAA.Continue Reading