Balozi Sefue aalika mawazo kuboresha makusanyo ya kodi

Balozi Sefue aalika mawazo kuboresha makusanyo ya kodi

Balozi Sefue aalika mawazo kuboresha makusanyo ya kodi

Moshi. Tume ya Rais ya Maboresho ya Mifumo na Muundo wa Kodi imewataka Watanzania kuwasilisha mawazo ya namna Serikali inavyoweza kuongeza ukusanyaji wa mapato bila kuathiri mazingira ya biashara, hatua itakayochochea ukuaji wa maendeleo.

Rai hiyo imetolewa leo, Jumatano, Januari 29, 2025, na Mwenyekiti wa tume hiyo, Balozi Ombeni Sefue, wakati wa mkutano wa majadiliano ya wadau wa kodi mkoani Kilimanjaro, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Moshi. Mkutano huo pia ulilenga kukusanya maoni na mapendekezo ya maboresho ya kodi.

Balozi Sefue amesema wigo wa ulipaji kodi nchini bado ni mdogo, huku wastani unaotakiwa kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara ukiwa asilimia 15 – 16, wakati Tanzania ikiwa katika asilimia 11.9, hivyo bado kuna kazi kubwa ya kuongeza makusanyo ya kodi.

Amesema kwa sasa kuna dirisha la wiki mbili, hivyo ametoa rai kwa wananchi wa Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla kuwasilisha mawazo yao kwa njia ya maandishi kuhusu namna ambavyo serikali inaweza kuongeza makusanyo ya kodi kwa kufuata misingi ya haki.

“Tuna kazi kubwa ya kuongeza makusanyo ya kodi kwa upande mmoja, lakini kwa upande mwingine, tunakusanyaje mapato kwa kuzingatia misingi ya kodi inayotambulika kimataifa?

“Msingi mmoja ni haki, kwamba nchi isiendeshwe kwa kodi za watu wachache—kila mwenye kipato alipe kwa kadri ya kipato chake, lakini alipe kwa namna inayotenda haki, yaani haki ionekane katika kukadiria kodi inayotakiwa kulipwa na haki ya mtu ya kusikilizwa malalamiko yake,” amesema Sefue.

Ameongeza kuwa, “Natoa wito kwa Watanzania wote popote walipo, kama una wazo zuri la namna gani tunaweza kuongeza kodi lakini kwa njia ambayo haitaathiri mazingira ya biashara, tafadhali tumia fursa hii kuwasilisha. Tuna dirisha la wiki mbili, tumia mifumo iliyowekwa ya kuwasilisha maoni.”

Changamoto za wafanyabiashara

Wakizungumza katika mkutano huo, baadhi ya wafanyabiashara na wadau kutoka sekta mbalimbali mkoani Kilimanjaro walikosoa baadhi ya mifumo ya ukusanyaji kodi, ikiwemo wa ukaguzi wa mahesabu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambao wamedai unawaumiza.

Jonathan Christopher, amesema ili kurahisisha ulipaji wa kodi na kuwawezesha wafanyabiashara kulipa kwa wakati, ipo haja ya TRA kuwekewa ukomo wa kufanya ukaguzi wa mahesabu ili kuondoa usumbufu.

“Tunawasilisha mahesabu TRA ndani ya muda uliowekwa, lakini baada ya kuyapokea, TRA inaweza kuchukua hadi miaka mitano kabla ya kuyapitia. Wanapoyakagua kwa wakati mmoja, mfanyabiashara anaweza kufanyiwa ukaguzi wa miaka mitatu hadi minne.

“Katika ukaguzi huo, mbali na kodi aliyopaswa kulipa, anaweza pia kutozwa adhabu kwa makosa ya nyuma ya miaka mitatu hadi minne, jambo ambalo ni mzigo kwa wafanyabiashara,” amesema Christopher.

Rajabu Msangi, amesema kumekuwa na changamoto katika ukadiriaji wa kodi, ambapo wakati mwingine husababishwa na baadhi ya wafanyakazi wa TRA wasio waaminifu, jambo ambalo huwaumiza wafanyabiashara.

“Kodi ni kwa maendeleo ya nchi na ni lazima kila mmoja apambane kutimiza malengo ya Serikali, lakini changamoto huwa inajitokeza wakati wa ukadiriaji wa mapato. Mfano, unakuta mtaji wako ni Sh10 milioni, unakuja kupigiwa kodi ya miaka mitano Sh20 milioni ilihali mtaji wako haufikii hapo. Hii ni changamoto kubwa.

“Tunaamini maoni tuliyotoa yatafanyiwa kazi na watakuja na mrejesho ambao utakuwa ni mstakabali mzuri kwa maendeleo ya nchi yetu,” amesema Msangi.

Kwa upande wake, Ibrahim Shayo amependekeza maboresho ya kodi ya huduma na kuomba wafanyabiashara kulipa kodi kutokana na faida waliyozalisha.

“Lipo suala la kodi ya huduma, tunatambua kodi hii ni takwa la kisheria, lakini tumekuwa tukitozwa kodi kutokana na mitaji tuliyo nayo, ambayo wengi ni mikopo ya benki. Tunaomba kodi hii ikafanyiwe maboresho na tukalipe kodi inayotokana na kile tunachozalisha,” amesema Shayo.

Katika hatua nyingine, Shayo amependekeza upanuzi wa barabara ya Tanga-Moshi na kupanua njia hadi nne ili kurahisisha usafiri na usafirishaji, hasa katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na ongezeko la mizigo inayosafirishwa kupitia Bandari ya Tanga.

“Naomba tuangalie hili la barabara. Kuna mikoa ambayo iko karibu na bandari, mfano sisi Kilimanjaro tupo karibu na Bandari ya Tanga, lakini barabara ya kutoka Tanga-Moshi kwa sasa imejaa malori na ni nyembamba. Ifike mahali turekebishe sheria na tujenge barabara za njia nne hadi sita. Hii pia itapunguza ajali na kuwezesha usafiri salama,” amesema Shayo.

Akizungumzia suala la upanuzi wa barabara hiyo, Balozi Sefue amesema ni wazo zuri, lakini akasisitiza ulipaji wa kodi.

“Wazo lako la kupanua barabara hii nalikubali kabisa, sasa tuongeze mapato ya serikali ili tuweze kujenga barabara,” amesema Balozi Sefue.

Oktoba 4, 2024, Rais Samia Suluhu Hassan alizindua tume hiyo kwa lengo la kuboresha ukusanyaji wa kodi, kuhakikisha ufanisi katika matumizi yake, pamoja na kushughulikia changamoto zinazoathiri mfumo wa kodi nchini.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Tanzania's opposition party ACT Wazalendo honours veteran politician under new policy
Tanzania Foreign Investment News
Investment News Editor

Tanzania’s opposition party ACT Wazalendo honours veteran politician under new policy

Unguja. Opposition party ACT Wazalendo today officially bids farewell to its former Chairman, Juma Duni Haji, also known as Babu Duni, as part of a new policy designed to honor retired senior leaders at a ceremony held at Kiembesamaki, Zanzibar.

The initiative highlights the party’s commitment to recognizing and supporting individuals who have served with dedication and integrity.

Babu Duni, who stepped down earlier this year, was succeeded by Othman Masoud, now the First Vice President of Zanzibar.

The policy aims to provide ongoing respect and support to retired leaders, ensuring their continued recognition and contribution to the party’s development.

“Recognizing their significant contributions to the development and prosperity of the party, this policy ensures that retired leaders continue to be acknowledged and respected by both the party and the community,” the policy states.

To benefit from this policy, leaders must not have left or been expelled from the party. They must have served the party with honor and dedication. The national leadership committee will determine whether a leader has fulfilled these criteria.

The policy seeks to honor retired leaders, protect their dignity, acknowledge their contributions, leverage their ideas for the party’s growth, and support them to the best of the party’s ability.

In honoring these leaders, the party will provide a vehicle, the type of which will be determined by the national leadership committee. Additionally, they will receive a monthly allowance, with the amount also set by this committee.

Other benefits include health insurance. If a leader does not own a home, the party will cover their rent at a rate decided by the committee.

The leadership committee may also grant special recognition based on the leader’s contributions. Retired leaders will participate in decision-making meetings according to procedures outlined in the party’s constitution.

Depending on the party’s resources at the time, the policy may also apply to retired deputy chairpersons for both the mainland and Zanzibar, the Secretary-General, Deputy Secretary-General for both mainland and Zanzibar, and the party’s Attorney General.

Additionally, leaders, executives, or members with exceptional contributions to the party’s protection, advocacy, and defense may also benefit, as determined by the leadership committee.

Currently, those who are eligible for benefits under this policy include Juma Duni Haji (retired party Chairman) and Zitto Kabwe (retired party leader).Continue Reading