ATCL’s cargo flights to China game-changing for avocado exporters
The maiden Air Tanzania direct cargo flight from Dar es Salaam to Guangzhou, China successfully commenced on January 12, 2025Continue Reading
The maiden Air Tanzania direct cargo flight from Dar es Salaam to Guangzhou, China successfully commenced on January 12, 2025Continue Reading
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo Januari 30, 2025 nchini Tanzania, hali ya waviu wasiotambua hali zao mpaka kufikia hatua ya kupata magonjwa nyemelezi (Ukimwi) bado ipo huku vijana wakitajwa kuathirika zaidi.Continue Reading
The registration will focus on new voters who have reached the age of 18, based on 2022 census data, and will require proof of Zanzibari identity.Continue Reading
The acquisition is Exim Bank’s third in six years.Continue Reading
The acquisition is Exim Bank’s third in six years.Continue Reading
This follows a review of budget performance in key sectors, highlighting progress in financial and physical targets for the 2022/2023 fiscal year.Continue Reading
Moshi. Tume ya Rais ya Maboresho ya Mifumo na Muundo wa Kodi imewataka Watanzania kuwasilisha mawazo ya namna Serikali inavyoweza kuongeza ukusanyaji wa mapato bila kuathiri mazingira ya biashara, hatua itakayochochea ukuaji wa maendeleo.
Rai hiyo imetolewa leo, Jumatano, Januari 29, 2025, na Mwenyekiti wa tume hiyo, Balozi Ombeni Sefue, wakati wa mkutano wa majadiliano ya wadau wa kodi mkoani Kilimanjaro, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Moshi. Mkutano huo pia ulilenga kukusanya maoni na mapendekezo ya maboresho ya kodi.
Balozi Sefue amesema wigo wa ulipaji kodi nchini bado ni mdogo, huku wastani unaotakiwa kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara ukiwa asilimia 15 – 16, wakati Tanzania ikiwa katika asilimia 11.9, hivyo bado kuna kazi kubwa ya kuongeza makusanyo ya kodi.
Amesema kwa sasa kuna dirisha la wiki mbili, hivyo ametoa rai kwa wananchi wa Kilimanjaro na Tanzania kwa ujumla kuwasilisha mawazo yao kwa njia ya maandishi kuhusu namna ambavyo serikali inaweza kuongeza makusanyo ya kodi kwa kufuata misingi ya haki.
“Tuna kazi kubwa ya kuongeza makusanyo ya kodi kwa upande mmoja, lakini kwa upande mwingine, tunakusanyaje mapato kwa kuzingatia misingi ya kodi inayotambulika kimataifa
“Msingi mmoja ni haki, kwamba nchi isiendeshwe kwa kodi za watu wachache—kila mwenye kipato alipe kwa kadri ya kipato chake, lakini alipe kwa namna inayotenda haki, yaani haki ionekane katika kukadiria kodi inayotakiwa kulipwa na haki ya mtu ya kusikilizwa malalamiko yake,” amesema Sefue.
Ameongeza kuwa, “Natoa wito kwa Watanzania wote popote walipo, kama una wazo zuri la namna gani tunaweza kuongeza kodi lakini kwa njia ambayo haitaathiri mazingira ya biashara, tafadhali tumia fursa hii kuwasilisha. Tuna dirisha la wiki mbili, tumia mifumo iliyowekwa ya kuwasilisha maoni.”
Changamoto za wafanyabiashara
Wakizungumza katika mkutano huo, baadhi ya wafanyabiashara na wadau kutoka sekta mbalimbali mkoani Kilimanjaro walikosoa baadhi ya mifumo ya ukusanyaji kodi, ikiwemo wa ukaguzi wa mahesabu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambao wamedai unawaumiza.
Jonathan Christopher, amesema ili kurahisisha ulipaji wa kodi na kuwawezesha wafanyabiashara kulipa kwa wakati, ipo haja ya TRA kuwekewa ukomo wa kufanya ukaguzi wa mahesabu ili kuondoa usumbufu.
“Tunawasilisha mahesabu TRA ndani ya muda uliowekwa, lakini baada ya kuyapokea, TRA inaweza kuchukua hadi miaka mitano kabla ya kuyapitia. Wanapoyakagua kwa wakati mmoja, mfanyabiashara anaweza kufanyiwa ukaguzi wa miaka mitatu hadi minne.
“Katika ukaguzi huo, mbali na kodi aliyopaswa kulipa, anaweza pia kutozwa adhabu kwa makosa ya nyuma ya miaka mitatu hadi minne, jambo ambalo ni mzigo kwa wafanyabiashara,” amesema Christopher.
Rajabu Msangi, amesema kumekuwa na changamoto katika ukadiriaji wa kodi, ambapo wakati mwingine husababishwa na baadhi ya wafanyakazi wa TRA wasio waaminifu, jambo ambalo huwaumiza wafanyabiashara.
“Kodi ni kwa maendeleo ya nchi na ni lazima kila mmoja apambane kutimiza malengo ya Serikali, lakini changamoto huwa inajitokeza wakati wa ukadiriaji wa mapato. Mfano, unakuta mtaji wako ni Sh10 milioni, unakuja kupigiwa kodi ya miaka mitano Sh20 milioni ilihali mtaji wako haufikii hapo. Hii ni changamoto kubwa.
“Tunaamini maoni tuliyotoa yatafanyiwa kazi na watakuja na mrejesho ambao utakuwa ni mstakabali mzuri kwa maendeleo ya nchi yetu,” amesema Msangi.
Kwa upande wake, Ibrahim Shayo amependekeza maboresho ya kodi ya huduma na kuomba wafanyabiashara kulipa kodi kutokana na faida waliyozalisha.
“Lipo suala la kodi ya huduma, tunatambua kodi hii ni takwa la kisheria, lakini tumekuwa tukitozwa kodi kutokana na mitaji tuliyo nayo, ambayo wengi ni mikopo ya benki. Tunaomba kodi hii ikafanyiwe maboresho na tukalipe kodi inayotokana na kile tunachozalisha,” amesema Shayo.
Katika hatua nyingine, Shayo amependekeza upanuzi wa barabara ya Tanga-Moshi na kupanua njia hadi nne ili kurahisisha usafiri na usafirishaji, hasa katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na ongezeko la mizigo inayosafirishwa kupitia Bandari ya Tanga.
“Naomba tuangalie hili la barabara. Kuna mikoa ambayo iko karibu na bandari, mfano sisi Kilimanjaro tupo karibu na Bandari ya Tanga, lakini barabara ya kutoka Tanga-Moshi kwa sasa imejaa malori na ni nyembamba. Ifike mahali turekebishe sheria na tujenge barabara za njia nne hadi sita. Hii pia itapunguza ajali na kuwezesha usafiri salama,” amesema Shayo.
Akizungumzia suala la upanuzi wa barabara hiyo, Balozi Sefue amesema ni wazo zuri, lakini akasisitiza ulipaji wa kodi.
“Wazo lako la kupanua barabara hii nalikubali kabisa, sasa tuongeze mapato ya serikali ili tuweze kujenga barabara,” amesema Balozi Sefue.
Oktoba 4, 2024, Rais Samia Suluhu Hassan alizindua tume hiyo kwa lengo la kuboresha ukusanyaji wa kodi, kuhakikisha ufanisi katika matumizi yake, pamoja na kushughulikia changamoto zinazoathiri mfumo wa kodi nchini.Continue Reading
Wakati awamu ya pili ya uandikishaji wa daftari la mpigakura ikitarajia kuanza Februari Mosi, Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo taifa, Othman Masoud amewataka wananchi wote kuitumia vyema awamu hii ya mwisho ya uandikishaji ili wapate fursa ya kupiga kura na kukichagua chama hicho kushika dola.Continue Reading
Serikali ya Ufaransa imeingia makubaliano na Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan ya miaka minne ya kutoa huduma ya chanjo ya saratani ya kizazi sambamba na matibabu ya saratani ya matiti kwa wanawake 800,000 Tanzania.Continue Reading
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, amesema mataifa ya Afrika yanapaswa kuuangalia ushirikiano wa China na Tanzania kama mfano wa maendeleo, akibainisha kuwa unatoa taswira ya maono ya pamoja kwa ajili ya mabadiliko, ustawi, na kisasa.Continue Reading
Zanzibar Investment News Tanzania Investors Ltd © 2025