Air Tanzania yashindwa kutua Bukoba, yarudi Mwanza

Air Tanzania yashindwa kutua Bukoba, yarudi Mwanza

Siku 11 baada ya ajali ya ndege ya Precision Air nchini Tanzania, iliyoua watu 19, Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeshindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera, kutokana na hali mbaya ya hewa.

Kwa mujibu wa Mwananchi Digital, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amethibitisha hilo na ndege hiyo ililazimika kurudi katika uwanja wa Mwanza na kutua salama.

Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira aliyekuwepo kwenye ndege ameandika kwenye mtandao wake wa twitter akieleza tukio hilo, na kutaka Serikali ibebe kwa uzito suala la uwanja wa ndege wa Bukoba.

From twitter

Novemba 6, 2022, Ndege ya Precision Air, iliyokuwa imebeba watu 43, ilidondoka katika ziwa Victoria, mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba, na kuua watu 19, huku 24 wakinusurika.

From twitter

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories