Afrika yakabiliwa na uhaba wa marubani,wahandisi

Afrika yakabiliwa na uhaba wa marubani,wahandisi

Arusha. Ushindani katika usafiri wa anga katika Bara la Afrika unatajwa kuwa mdogo kutokana na mashirika ya ndege kuwa machache na kuwa yakiongezeka yatasaidia kuongeza ushindani,nauli kushuka pamoja na ubora wa huduma kuongezeka.

Aidha,  bara hilo linatajwa kuwa na upungufu wa rasilimali watu wakiwemo marubani na wahandisi katika sekta hiyo muhimu ambayo inazidi kukua kwa kasi.

Kutokana na sababu hizo,  wakurugenzi wakuu na wakuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Afrika ( AFCAC), wanakutana jijini Arusha kwa siku mbili kujadili namna ya kuboresha sekta hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo leo Jumatano Juni 5, 2024, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa anga nchini (TCAA), Hamza Johari, amesema  malengo makubwa ni kuweka mikakati ya pamoja katika bara hilo kuhakikisha usafiri wa anga unakuwa salama.

“Tunataka tuangalie masuala ya kiushindani katika usafiri wa anga,tumeona kwamba ushindani si mkubwa sana kwani mashirika ya ndege ni machache,yanapokuwa machache nauli nazo zinakuwa juu tunataka yawe mengi,yanavyokuwa mengi yakashindana vizuri basi nauli na zenyewe zitarekebika.

” Tunataka tuangalie masuala ya rasilimali watu kwa maana ya kwamba tuna upungufu wa idadi ya marubani wanaohitajika katika sekta upungufu wa wahandisi wanaohitajika pia,”amesema Johari.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Oktoba 5, 2023 mkurugenzi huyo, amesema kuanzia mwaka 2003 hadi 2023, idadi ya ndege zilizokuwa zinatoa huduma katika anga la Tanzania zimeongezeka kutoka 101 hadi 206,marubani wakitoka 234 hadi 603 huku waongoza ndege wakiongezeka kutoka 70 hadi kufikia 154.

Amesema kulikuwa na ongezeko la wakaguzi wa usalama kutoka 28 hadi 44, wahandisi wa mitambo ya viwanja wakiongezeka kutoka 20 hadi 44 na wataalam wa anga wakiongezeka kutoka 50 hadi kufika 83.

Kuhusu marubani amesema Tanzania inahitaji marubani 780 hivyo kuna upungufu mkubwa kuendana na kasi ya ukuaji ambapo hadi wakati huo walifadhili marubani 22 waliokuwa wakisoma nje ya nchi ila kwa sasa NIT itafundisha kwa Dola 48,000 ambazo ni sawa na Sh120.3 milioni badala ya Dola 120,000 zilizokiwa sawa na Sh300.9 milioni.

Hatua nyingine ni kuhakikisha usafiri wa anga Afrika unazidi kuwa salama na endelevu na kuwa wataangalia eneo la ulinzi kwani kumekuwa na tabia ya watu wenye nia ovu ikiwemo magaidi,kuteka ndege, kulipua viwanja na kutega mabomu japo matukio hayo hayatokei kwa wingi katika bara la Afrika lakini lazima wachukue tahadhari.

“Sasa hivi dunia imekua katika teknolojia kila kitu kinakwenda kidijitali na tunavyokwenda kwenye ulimwengu huo kunaweza kutokea mashambulio ya mifumo na mifumo ikiharibika tutashindwa kufanya shughuli zetu,tutaangalia zaidi uhalifu huo wa mitandaoni ili tusije kushambuliwa na tutengeneze sauti moja kama Afrika,”ameongeza Johari.

Akifungua mkutano huo, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema wakuu hao watajadiliana na kutoka na maazimio ya pamoja katika kuboresha usafiri huo pamoja na miundombinu huku suala la usalama likipewa kipaumbele kwani bila usalama hakuna usafiri wa anga wa uhakika.

Kuhusu suala la uchafuzi wa mazingira,Waziri Mbarawa amesema wakuu hao na wataalamu wa sekta ya anga watajadiliana jinsi wanaweza kuhakikisha anga linakuwa safi na salama na kuongeza maendeleo katika nchi hizo.

“Tanzania tumefanya kazi kubwa kwenye sekta ya usafiri wa anga na tuna miradi mbalimbali inaendelea na lengo la Serikali ni kuendelea kufungua usafiri wa anga na kuifanya anga zetu ziwe salama.

“Tunaendelea na ujenzi mkubwa wa viwanja vya ndege katika mikoa mbalimbali ikiwemo kiwanja cha Msalato Dodoma ambacho kitagharimu zaidi ya Sh365 bilioni,”amesema.

Waziri huyo amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha mikoa yote inakuwa na viwanja vya ndege vya kisasa na kuwataka Watanzania waendelee kutumia usafiri huo ambao ni usalama zaidi ukilinganisha na usafiri mwingine.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Popular
Chief Editor

Insecurity prompts Zanzibar to review its lucrative island leasing

The Tanzanian central government is planning to boost its security presence in the Zanzibar archipelago. A commission tasked with auditing the country’s security forces was appointed in July by President Samia Suluhu Hassan. It says it is concerned about the situation in the country’s Indian Ocean islands that are under the control of the semi-autonomous Zanzibar local government.Continue Reading